KISIMANI TUTAKUNGOJEA

Mwaikoma G. A

SHOMBO2

kanga , Vazi Mashuhuri La Africa Mashariki
kanga , Vazi Mashuhuri La Africa Mashariki

Lazima niseme neno, hata kama kwa kalamu ya shombo, kwani majununi vijana waleo: wamekosa maungamo! Ndugu na jamaa wengi walowatangulia kwa huzuni wamefariki dunia, walobaki Kama Mama ndege alopoteza yake makinda. Tumebaki sisi wachache vizazi viwili katikati , tukiuchungua ukweli kutoka zote  pande ! Na maisha yetu ya upweke: hatukuwaona Wajomba, Bibi, Mababu Mashangazi, na wengine wengi Wapenzi. Ye mwache alete dharau’ Lakini kwetu siye kazi. Na mchezo huo hata siye tunauweza’ Kama ye aruka, siye twatembea’ Kiu kitapomshika, chini kisimani atarejea’ Kuruka warukaruka kimekushika kiranga cha anga. Halibishiki moja ndege mjanja: huwezi kunywa matoneni mwa mvua huku waruka’ Hivyo basi chini utakaposhuka: Kisimani tutakungojea. Jinyama lisilo julikana, mayai viza limeatamia, Muhula unapofika kama mabomu yanalipuka’ ndugu usiombe kukutwa mhanga. Vinyongo na chuki, vijifundo vya gubu na uhasidi nafsiyo vitairarua! Lakini kumbuka la samaki shombo lanuka hata hivyo nazi tutamkunia na kitoweo chake kitamu twapendelea. Akikwambia bayana kwenye nyumba za watu hapendelei kula iweje kwake akusonga sana kukupikia? Kweli harufu ya mbwa unaijua mzoga, watembea mzima iweje akuambie umeoza? Masihara hayo tayari amesha kukua’ kifuatacho wala si kikao cha mgonjwa bali jina marehemu kukubatiza! Eti shimoni wamekuja nitembelea, salamu yao: Vipi’ Hivi bado tu hujafa? Mtavunja hewa za moto,Mulungu amenishikilia. Maji utakapokuja kunywa’ kisimani tutakungojea.

egypt8

Kwenye Jumba la masahibu, usijifanye Msharifu, Kasisi wa Upendo na amani kule ghaibu, huku kayani umetuacha mahameni’ Mara ya mwisho sijui alikanyaga nani. Kwani hapafikiki, kulupukulupu za nini, vikumbo na majoka, mijibundi na manyang’au ya usiku. Ni uhasama ulozi mpaka kwa makinda yasiyo na hatia. Kisha wana mnadi Muumba kwa uharamia na mitutu: Ugwiji kwenye nchi za watu! Al – Mashuhur Sina Mungu. Shimoni waja nitembelea, kisha wakasirika kwanini bado sijafa? Mhindi wala hakukosea Lugha’ aliposema: menyewe kwa menyewe inauana! Baba mzima tena unalea wana, chunguni kuiba mboga! Hii kweli inatafakurika! Hasa yathibitisha wewe jando hukulipitia! Au yule mwana alo mtaka Babake urithi  akingali hoi kitandani, Mzee akamjibu utatangulia wewe mwanangu! alipotoka nje ya jengo tabibu akagongwa gari akafa yule kijana! Kiu kitapowashika’ Kisimani nitawagojeeni. Kama umemaliza kulea, Shukrani mpe Mola. Utoto wako huwezi kumbuka, napi na makalio yako ni nani alokusafisha! Uzazi ni malezi usijinadi kwa urijali. Nipe muda kidogo samahani, nasafisha napi za mwanangu! Na kwa habari za Mke wangu kikongwe’ wala usisumbuke’ Miye mwenyewe Mbishi hadi kuvunja miiko ya Ufalme wa Useja. Aijuae Ndoa katu hatomkasoro mke wa mwenzie, kwani anaijua kasoro ya wa kwake: Ni vijana hawa mapengo, ndio waropokao, Nasi Kisimani twawangojea; watakapoleta vyungu vyao! Wakunga msiwatukane , na uzazi ungalipo, wala Mamba kuwakejeli kabla ya kuuvuka mto, la sihivo masihara masihara yenu huleta dharau hadi kwa  Muumba. Matokeo yake nini: Dume zima linalilia kuolewa! Basi Binti yangu alipovunja ungo wakampeleka Mkoleni, huko ni kama jando, watoto wa kike kupokea mafundo, mara dume moja likajipitisha hata haijulikana wapi liliko tokea, Makungwi wakalikamata kulikabidhi kisago kwa ghafla: likakimbia na kutokomea huku likidai samahani nilikuwa natania!  Mwanangu mwenyewe Mboni, Chini ya Ulepe wa Jicho Langu KipenziMwanangu kwani wapi umemkanyaga Mumbi, Tanzia yote na mikosi kukuandama! Hicho kizingiti cha mikosi ni wapi ulipokiruka? Watasingizia upepo na maji: Ukisha sikia hivyo tu umekwisha, Itakuwa Buriani: lakini siburee’ Kuna mkono wa mtu. Mkumbuke Mulungu wako atakunusuru, kisimani wao wenyewe watarejea.

SHOMBO3

Asanteni sana

Gamieri Ahadi Mwaikoma

Njiwa Mweusi”

Malenga wa Isusi

Leave a comment