TUKAZUGE ULAYA

Gamier  Ahadi Mwaikoma

KEM2

MAUNGAMO

Watu wengi sana wanatamani kwenda kuishi Ulaya. Ulaya kuzuri, kwenda kwa  wazungu ni ndoto ya wengi. Kuwavusha watu Ulaya ni Biashara Kubwa. Kuna wale tukajipatia mabibi(Dizaini nikisha seto namtosa…hahah utatoswa wewe!! Kumradhi- sio wote tu ili wakaishi Ulaya-yako mapenzi ya kweli) Wako waliokwenda na kutokomea huko. Wako waliorudi na hawatamani kurejea katu! Sasa uhamiaji ni tatizo kubwa Ulaya. Sio tu Weusi wagombanao kwenda Ulaya, hata Wazungu pia wa Ulaya mashariki na kwingine maskini waliokumbatia Siasa na sera za Kijamaa. Ndipo inatubidi tufafanue maana ya Ulaya, au Ulaya Magharibi. Majuzi hapa tumeshuhudia wahamiaji wakipata ajali, na kutelekezwa baharini! Watu wanataka kwenda Ulaya Bwana.

Ulaya ni bara la Pili Kwa Udogo ki kilometa mraba yaani10,180,000 ambazo ni 3,930,000 mitamraba ambazo ni 2% za tufe la Dunia na 6.8% ya ardhi yake.Ulaya ni mkusanyiko wa Nchi 50. Urusi ndio Kubwa kuliko zote ikichukua 40% ya Bara Hili, na Vatican ndio Mji Mdogo Kabisa. Ajabu Ulaya ndilo Bara la Tatu Kwa wingi watu waishio, baada ya Africa na Asia, Karibu watu 800 millioni.[1] Inadaiwa na Kukubalika Kwamba Kitovu cha Ustaarabu Wa Ulaya Magharibi ni Ugiriki[2], heheheh…nicheke miyee..kwa mafilosofa wenyewe..Au Siyo?

SHOMBO3

Ulaya ninayoizungumzia ni kitovu cha mfumo wa Kibepari, na Nchi wadau wake pia walishiriki Biashara ya Utumwa, Ukoloni na kitangulizi chake ile waliita biashara Huria! Nchi za Ulaya kinyume na zingine zinatambulika kwa uchumi wake mnono, taratibu thabiti za kitawala na uchumi, msisitizo katika haki za binadamu. Ulaya inatuathiri kwa kila namna! Kidini, kiuchumi, kihistoria, kisiasa nk. Ulaya ndio mdau mkubwa kabisa wa Tengenezo La Dunia ya sasa. Sasa hili si andiko la somo, bali mchezo wa kuigiza. Hatahivyo tuliwajibika kufanya utafiti ilikutamthilihisha ujumbe huu vizuri. Ni ajabu ambavyo sehemu hii ndogo katika Tufe la Dunia imekuwa na nguvu kuu mno katika maisha ya Tufe zima kuanzia karne ya 15 na Kuendelea wakatawala karibu dunia nzima kibabe!. Lakini mapinduzi ya Viwanda karne ya 18 ndio hasa yalileteleza tofauti kubwa na athari kwa dunia nzima kama tuijuavyo leo[3].Kwa mfano nikichukua kipengee cha Dini tu, yaani kama wewe ni wa madhehebu ya Kikiristo basi u malighafi ya umbiko wazo la Ulaya. Hapa tunaibua hoja kwamba dini ni kitendea kazi, ni silaha yenye nguvu mno kuliko bomu la nyukilia! Sasa kuanzia mwanzo wake, kazi hii tulikusudia iwe ya kuleta mabadiliko (Revolutionary Theatre). Kuwafikisha mahali watu weusi kama walengwa na wakusudiwa, wakajitathmini upya, na mustakabali mzima wa Utu na Bara lao. Tunaishi katika nyakati za hatari, roho ya mweusi inapotea kabisa. Hujui unachopigana nacho! Sio ubepari! Na wala ujamaa sio suluhisho! Bali kujitambua, na kile unachokabiliana nacho, yaani kuvuliwa utu wako, ni kama kuchunwa ngozi vile! Hutasalimika! Ngugi WaThiong’o , Chinua Achebe na wengineo wamepigania urejeshwaji wa Kumbu kumbu hifadhi la utamaduni. Vinginevyo Tumeishia kuwa vitendea kazi na wawezashaji tu kwenye  Jukwaa la Wachuna Ngozi. Au kama vipi,twenzetuni wote tu, Tukazuge Ulaya…au siyo??? Unapoukana utu, wako, ukavaa wa mwingine, mbele zake yule we huwi binadamu aliyekamilika! Sasa kakupa Jina la Bara lako eti Africa, umekubali, jina lako Binafsi, Abdallah na Godffrey, umekubali, kakupa na Elimu sasa hadi kukutambulisha we kwa nafsi yako mwenyewe. Kuna kilichobaki? Ile wanasema kustaarabishwa: Lakini asiyestaarabika nani? Mtu nusu? Si yule asiye na Mungu wake anaabudu Miungu ya wenzie. Miungu yake inamlilia, inamwomba aikumbuke, Ye haaaa, kaikana, kaambiwa na kaamini miungu yake ndio Mashetani. Utamfanya nini mtu huyu, kama maiti basi hana budi kufufuliwa. Tazama tamaduni , mila,Dini na desturi za Uchina , India. Imani Kongwe kuliko Uislamu na Ukristo. Na Mabara haya yanatoa changamoto kubwa sana kwa Ulaya. Mweusi ye haa! Hana jina, hana kwao, hana dini, hana lolote! Wamebaki kunyanyasa watu wao, kudhalilisha mamlaka, na kubugumya rasilimali zao wenyewe. Sasa siye wakina Kiokote tufanye nini? Si tukazuge tu Ulaya?

Asanteni sana na wote mnakaribishwa basi katika zoezi hili la kumfufua maiti huyu.

G. A. Mwaikoma

Tamthiliya zingine Za Mwandishi ambazo bado kutolewa ni:

MUMIANI

WACHUNA NGOZI

Massoud Ukingali: We Unakujua Ulaya? Unapafahamu au una Pasikia? Au unapaona kwenye runinga na kwenye filamu za Kuigiza? Mwanichekesha sana vijana kizazi kipya, Cha Hipu Hopu na Ponographia.

[1]  “World Population Prospects: The 2012 Revision“. UN Department of Economic and Social Affairs.

       [2]   Lewis, Martin W.; Wigen, Kären (1997). “The myth of continents: a critique of metageography”.   University of California Press

       [3] Ibid. 2

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s