ON THE CONCEPT OF GOD

THE GLYPHS: SACRED WORDS (VIELELEZO VITAKATIFU)

G. A. MWAIKOMA

SEHEMU YA KWANZA

MIKATO: THE GLYPHS

MIKATO2

 UTANGULIZI

VIDONGE VICHUNGU

Kwanza kabisa  nitubiye, baadhi ya mambo yatakayo semwa humu ni vidonge vichungu, wengi watakwazika na kukasirika, lakini chungu dawa, walishasema mababu. Tukimeza au tukitema hiyo ni shauri yetu! UKWELI HUWA UNATABIA YA KUKATALIWA:  mwishowe unabakia kuwa ukweli.

Insha hii inatoka katika kazi zangu kadhaa za awali, hasa “HEKALU LA MULUNGU”. Ama THE KHEMET TEMPLE’ Nilipoiandika  Insha ya” RAISI KIONGOZI MWONGOZO”, nilikusudia kuwasaidia viongozi wa bara la watu weusi (Khemet) kufanya uongozi mwema na kulikomboa bara lao ambalo limepuuzwa na na kusetwa kwa maelfu ya miaka sasa, pia kutatua tatizo la mtu mweusi. Aidha Insha hii sasa ni kitabu kimekamilika na niombi langu kisomwe na Viongozi wa Bara lote la watu weusi au Khemet ( Africa)

Bila shaka mweusi ni tatizo, Tukubaliane katika hilo! Lakini chanzo cha Tatizo ni Imani hizi za Kigeni ama Ukristo na Uislamu makinda ya Ujudaism! Nilipokuwa nikifanya utafiti wa kazi hii ndipo nikang’amua haya: Kwamba ‘ uongo ni uongo tu hata uupake vipi rangi ya ukweli utabakia kuwa uongo’  Nimeteseka mno maisha yangu nikijaribu kujitambua na kujielewa mimi ni nani? Na nikaweza kupata baadhi ya vidokezo kwamba mtu mweusi unamtambua kwanza kwa imani yake: Muislamu au Mkristo, pili Kumbu hifadhi lake linaloibua ustaarabu wake na ajali yake katika ulimwengu huu wa sasa. Wengi wetu weusi hatuna majibu, kwamba kwa nini tuko tulivyo? Sisi ni watu walioikana asili yao, kwa kujua au kutokujua. Tatizo la mweusi ni kujikana mwenyewe au Denial! Nakiri tatizo hili lilinisumbua tangu kuzaliwa na wazazi muhanga wa tatizo lile lie..!, sasa miaka 36 nashukuru  kwa kuamini nimeupata ukweli SASA. Ukweli kwamba mtu mweusi anayo asili na utu wake jambo ambalo katu halina mjadala! Masikini wa mali lakini tajiri wa roho. Mweupe mwizi, tajiri wa mali lakini maskini wa ROHO. NA MWENYE KUTAKA MALI ATAIPOTEZA roho yake., Kama alivyokwisha kusema Yashua Mwalimu mkubwa wa Fumbo jipya: Agano jipya kama mnavyoliita na kulitambua wengi wenu. Imani ni fumbo ama coded message! Ubepari ni wizi uliohalalishwa, ni wizi tu ambapo wachache wanafaidika kwa nguvu kazi ya wengi! Mweusi akitaka kukomboka kwanza atakabiliana na Uyahudi, pili Ukristo, alafu Uislamu. Ndio vitu vimbainishavyo. Cha mwisho ambacho ndio asili na cha kwanza ni imani na ibada yake ya asili: Imani kwa mababu  yaani mizimu yake. Nami nilikabiliana navyo. Kama Mkristo, Rasta, Muislamu, Atheist  kwa maana ya (Mso Mungu ama mkana Mungu) na Hatimaye Muumbile au muundo umboji( formist) Ndio naamini katika maumbo  kwa maana ya ibada ya wahenga, ni maumbo matakatifu na ndio dhana ya Mungu ilikoanzia na darasa letu la leo.

URASTA/ RASTAFARIANISM,

“Kwanza kabisa ni hatari kama mtu anakufahamu , alafu wewe humfahamu’ kwani daima atajua hatua yako ya pili unakanyaga wapi, nawe hujui yeye yuko wapi”*[1]

Urasta ulipokutana na ngano za Kiyahudi ukapoteza njia. Si walaumu , Bob, MARCUS GARVEY NA WENGINE WALIOSHADADIA NGANO ZA WAYAHUDI KUWAUNGANISHA NA BARA LA KHEMET. Sasa tunajua kisayansi si za kweli. Huzuni kubwa ni kwamba ustaarabu mkongwe wa dunia wa Khemet ulivunjwa vunjwa chini vipande na Ngano hizi zA JAMII YA WATU AMBAO MAELFU YA MIAKA KABLA DUNIA KUWAFAHAMU KILE WALICHO KINAJISI KILIDUMU. MYAHUDI MWONE KAMA ALIVYO: JAMII  NDOGO YA WATU WA JANGWANI WA SEMITIC  WAKAUVUNJA USTAARABU ADHIMU ULIODUMU KAMA MWANGA WA DUNIA KWA MAELFU YA MIAKA NA KUONGOZA NJIA YA USTAARABU WA DUNIA YA LEO. WAYAHUDI WAKAUPINDUA KICHWA CHINI MIGUU JUU! LEO WATU HAWAKUMBUKI KHEMET BALI WAYAHUDI NA HADITHI YAO YA UONGO, AMBAYO IMEKOSA MASHIKO YA KIAKOLOGIA NA SAYANSI KWA UJUMLA.

Sasa unaposhughulikia suala la ukombozi wa mtu mweusi Rasta ndio hatua ya kwanza katika wakati huu wa sasa/ Modern times. Kwani Rasta ndio falsafa iliyo kamilika ikiwa na lengo mahususi la ukombozi wa mtu Mweusi. LAKINI WHAT IS RASTA? Rasta ni kitu gani? It’s now a popular culture coinage, with reference to Bob Marley and the Wailers. Na ni kweli kabisa Bob Marley alikuwa nguvu isiyokanika ya utetezi wa mtu mweusi. Lakini samahani kwa donge chungu hili: kwangu mimi Bob Marley hakuwa Rasta, Kama ni mtihani alishindwa! Alijaribu kuwa rasta lakini alifeli.  Bob Marley alitelekezwa na Babake Bwana Marley,mpaka miaka michache kabla ya kifo chake daima alijibainisha na weusi[2].Lakini Bwana Blackwell producer wake alipokuja na mkataba mnono wenye kulinda maslahi ya weupe akimwambia lazima uwe kiongozi wa bendi, ndipo Bob akaonyesha rangi zake halisi sasa, kama fisi na nyama. Mtu mweupe mali Bwana, hapo utamuua! Anatamaa nyingi mno! Angalia Kumbu Hifadhi lake lote daima ni kuvamia , kuvunja na kuchukua, si tu mali bali na mawazo: Kisha anayaharibu na kujifanya ye Bingwa.  Nyuma yake akiacha mkorogo  wenye mchanganyiko na mashaka makubwa, ambayo hatimaye hurudi kumuumbua! Alipo mwambia we una damu ya weupe Semite au Semi-white na hiyo ndio itauza kiwandani Bob akaanguka hapo. Tamaa! Peter Tosh Hakuanguka. Alibishana na hatimaye akajiondokea zake na Bunny Wailer. SHETANI YULE YULE WA ZAMANI

Hapa sasa tunafumbua fumbo  moja wapo la bustani ya Edeni: Hivyo Bob Marley alikuwa kama Eva, lakini Tosh alikuwa Adam. Tosh alikataa kurubuniwa.

 bunny wailer and tosh 2

 Bunny Wailer and Tosh: The true revolutionaries!

 Wale waliokuja Baada na kumsikiliza Bob Marley leo wanajuta! Bendi imevunjika , mali yote iliyotolewa mahususi kwa kwa agenda ya ukombozi wa mtu mweusi imeishia kwenye familia ya Bob Marley. Kwani Bob hakuwajumuisha katika mkataba ule mnono ambao sasa unakisiwa kuwa zaidi ya Dolari bilioni 1.[3] Sio unakenua meno hapo Bobu Bobu, mwenzio kauuza utamaduni wako!     Na kibaya Zaidi kuthibitisha hili, mmoja wapo wa wanae Bob: Zigi hivi karibuni amenukuliwa kusema anatafuta asili yake ya Kiyahudi kutoka kwa Bibi yake mkubwa Mamaye Babake Bob[4] ETI ANADAI “ Naonea wivu utamaduni wa Kiyahudi” Can you imagine a Rasta saying That? Kwanini asiuonee wivu utamaduni wa Weusi? Kwa kusema hivyo Ziggi anathibitisha yeye sio mweusi. Na Kwanini sio? Dhana ile ya Kirugaruga[5]  au Maumau ya watu weusi ilipofika Ulaya kupitia picha kwenye Magazeti ya Kiingereza zilizoonyeshwa kuuliwa kwa Viongozi wa Maumau, wafungwa watu weusi wakiwa na manywele marefu mpaka miguuni, Watu wa Mungu waliokula viapo kupigana hadi kufa kuitetea Nchi Nyeusi , utu na utamaduni wao, Uingereza na Ulaya walitaharuki, mabibi na Mabwana,wazee kwa watoto. Sasa British West Indies na Carribea vijana wakavutwa na waruga ruga wale. Wazo lile likagongana na dhana za Marcus Garvey, Mweusi huyu aliyeibebea kichwa kichwa hadithi ya Musa na Suleimani kuhusu ndoa yake na Binti mzuri mweusi au Malkia wa Sheba, na kuacha vizalia huko Kush( Ethiopia ya leo) Hadi sasa na ndipo Urasta ukachanganyika na Uyahudi hapo. Si walaumu nikutokujua. Marasta wengi walimeza tego hili kama wengi wetu leo. Bob Marley Mwenyewe aliutukuza utamaduni wa Kiyahudi. Nyimbo zake nyingi ameimba kuhusu Mlima Sayuni(Zion) na kumtukuza Simba wa Yuda( The Lion of Juda). Leo hii tunafahamu kisayansi kwamba Hadithi ya Wayahudi bara la weusi haikutukia! Ni uongo mkuu sana uliopata kuandikwa. Na Rasta ikapotelea hapo.Dhana yoyote inayojaribu kumtukuza mtu mmoja Zaidi ya mwingine kwa damu yake ni ya Kishetani! Wayahudi kikundi cha kikabila cha watu wa Jangwani wenye asili ya Kiamori kweli walikuwepo Khemet, kama mataifa mengine waliokwenda kujitafutia maisha kule , kwani palikuwa pamestaarabika mno kwa viwango vya dunia ya wakati huo.Wagiriki kwa warumi, wasiria na wengineo[6].  Kama wakina siye tukigongana vikumbo vyetu kuja Ulaya leo! Babu zetu waliwatendea wageni kwa haki zote wala hawakuwanyanyasa. Watumwa kama ilivyoada walikuwa waasi , na mateka wa kivita. Vinginevyo raia wema walipewa haki zote hata kuwa viongozi kwenye serikali ya Khemet. Kakabila haka kadogo kama ilivyoada ya  mnyonge na ndoto zake kakabuni hadithi hizi kupitia ma scribes au waandishi ili kujifariji. Lakini ngano hizi zimekuwa na athari kubwa mno kwenye dunia ya Leo, ikiwa ni pamoja na mchango wake katika biashara ya utumwa na Ukoloni. Mambo waliyoyafanya Wakristo na waislamu wakiamini Khemet walikuwa watu wabaya waliostahili adhabu kwa mujibu wa ubaya waliowatendea Wayahudi. HADITHI HII YA Wayahudi haithibitiki kwa mujibu wa KUMBU HIFADHI YA iliyothibitika leo. Lakini Khemet imethibitika tena na tena na milele. Babu zetu katika majengo ya mapiramidi na masanamu mengine waliacha sahihi yao kama Ushahidi wa Kumbu hifadhi LAO! NDIO SABABU HAISHANGAZI kukuta Historia ya wayahudi sio TAALUMA bali theologia. Haiko katika Historicity wala haina mashiko ya kiakiologia. Unaikuta katika idara za kidini za vyuo vikuu.

Waandishi wa Agano la Kale walikuwa wanaigiza na pia wakiwa na agenda mahususi ya kuchafua fahari ya kitaaluma, falsafa na Imani na Dini ya Babu zetu. Nawamefanikiwa sana katika hilo. Kwani leo mtu mweusi amefikia mahali haamini tena katika nafsi yake, wala kilicho chake. Daima anaamini kikipitishwa na Mweupe ndio sahihi. Si tu agano la kale hata jipya pia lina matatizo yake. Katika kubatizwa kuwa mkristo unafanyishwa tambiko  la kikristo na kuapishwa kuikana nafsi yako ya zamani! Ndio mzizi wa fitna na uchafu na uharibifu uliko anzia. Lakini tunajuua Biblia kwa maana ya Agano la  Kale ni ngano za mascribes wa kiyahudi, tena mambo mengi yanaakiasi ustaarabu na mafunzo ya Babu zetu waliyo kopipesti. Agano jipya ni mradi mahususi ambapo watu walikaa, wakachagua , kuhakiki na kupitisha kitu ambacho kinaitwa Agano jipya leo kwa agenda zao Binafsi za kitawala. Na wamefanikiwa mno katika hilo. Kwani kadri mweusi anavyoshikilia Imani hizi,daima atawatumikia mabwana hawa weupe, atakauwa chini yao. Chini ya utawala wa Roma na Maagizo ya Mfalme Constatine, waheshimiwa hawa walikutana wakalisuka agano jipya na kuunda Imani ya Ukristo kwa maana ya Roman Catholic kama tuhifahamuvyo leo[7]. Na mafundisho ya Uungu wa Yesu na utatu mtakatifu. Sasa tunajua Wayahudi hawalitambui Agano hili jipya wala Ukristo. Na marasta vivyo hivyo. Lakini kwa ufahamu wetu sasa hata la kale si salama, ukweli wake na hata kuwepo kwa Musa kuna bishaniwa. Iwavyo vyote Vitabu hivi chini ya kanisa ndio vimekuwa msingi wa utawala wa dunia ya leo, kama ilivyokusudiwa na Bwana Costantino Al-maarufu mkuu . Bob Marley amepata kunukuliwa akikosoa nakala ya King James ya Biblia, akihoji usahihi wa kuwepo kwa jina la mfalme huyo kitabuni na kudai ni maneno ya Mungu. Si tuhapo, katika wimbo wao the Wailers uitwao Get up, Stand Up, ambapo bila shaka watu weusi waliitwa kusimamia haki zao, wakiagizwa watoke makanisani  NA KWENYE iBADA ZINGINE ZOTE NGENI’ kuna mistari inayomkana Yesu waziwazi, wanaposema:

Preacher man don’t tell me heaven is under the earth I know you don’t know what life is really worth Is not all that glitters in gold and Half the story has never been told So now you see the light, aay Stand up for your right. Come on

Na Pia;

Most people think great God will come from the sky Take away ev’rything, and make ev’rybody feel high But if you know what life is worth You would look for yours on earth And now you see the light You stand up for your right, yeah!

Na mahususi kabisa:

We’re sick and tired of your ism and skism game Die and go to heaven in Jesus’ name, Lord We know when we understand Almighty God is a living man You can fool some people sometimes But you can’t fool all the people all the time So now we see the light We gonna stand up for our right

Hawakuwa mbali na ukweli huu, lakini hawakuwa salama katika Ujudism pia. Na wakipambana na Ukristo, wanasahau mchango wa Uislamu kufuta kumbu hifadhi ya Imani za weusi vilevile. Pia hawakujua kwamba kabla Ya waisraeli, Babu zetu walikuwa na Imani thabiti katika si tu Mungu mmoja bali Miungu. Sasa tunafahamu  hata Uislamu ulikuwa ni mradi wenye agenda yake binafsi pia, Ikikopa kutoka Uyahudi, Bwana Muhamadi alikaa na Jopo la watu kuandika Kitabu chake. Miongoni mwao Kasisi aliyeasi wa Dhehebu Katoliki. Nikibishana na waheshimiwa Fulani kuhusu Imani ya weusi wakaja na hoja kwamba, Nyinyi hamna Kitabu. Hamna imani ya Kwenu , mnakopa tu za watu. Nikamjibu sisi tunayo , tena Kongwe, nyinyi ndio mmekopa kutoka kwetu. Babu zetu waliandika moja ya maandiko ya Kale Zaidi: KITABU CHA WAFU[8]: Ambacho pamoja na Mengine ya mawaidha ya Maisha, kilimwandaa mtu katika safari ya Maisha yake baada ya Kufa.

wafu

Kielelezo Katika Kitabu cha wafu

Hata dhana ya hukumu kadri ya Matendo yetu ni ya Weusi kwa maana ya mioyo itawekwa kwenye mizani.

Imani ya weusi haina mahusiano yoyote na wageni wa Bara la Weusi wowote wale, Si weupe wala nusu weupe, wala Waarabu wala Waisraeli, wala Warumi wala wagiriki.  Mtu mweusi rejea njia yako ya asili, ilikuwa safi na takatifu.

 1334424152_Bob-Marley

 Robert Nesta Marley  Mfanya Biashara wa Imani ya Weusi

Na jasusi la Ujudism

Alianza kama Rasta lakini hakufa HIVYO!

Kwanza Rasta yenyewe ni upotoshaji. Inawafanya weusi wasikumbuke Imani zao za asili na kuziendeleza.  Badala yake kuunga mkono ukuu wa dini nyeupe za kigeni dhidi ya weusi[9] Kama wenzie Uislamu na Ukristo, Weusi watoke katika zote hizo na kurejea Imani zao za asili. Ili iwe ngome Ya Ukombozi Rasta lazima irejee urithi wa zamani wa Kiimani wa Mababu weusi wa Kush na Khemet. Ukifumbua fumbo Rasta ni imani ya Mungu mkongwe  wa Kikemet RAA!

Asili ya Rasta ni weusi waasi   wa  Bara la weusi na si tu Kenya kama wengi wanavyodhani! Lakini Waasi hawa pale Kenya ndio waliobainisha Rasta kama tunavyoijua leo! Ambao walisimama kupinga dhuluma ya mwingereza na utamaduni wake wa kikoloni, na Ngugi Wathiong’o hawezi kukwambia hilo: kwani anatafuta utukufu wake mwenyewe!  Na si peke yake kuna wenzie wengi tu, watu tuwaheshimuo, waliopata nafasi kubwa ya kuusimamamia ukweli, lakini kwa kujua au kutokujua wakaangukia mtego ule ule!!!! Hakika shetani ni kiumbe cheupe kwani ni Bingwa wa mitego au matego!!

ngugi2

Ngugi Wathiong’o: Amejaribu katika andiko lake a KU-Ikumbuka Africa( Re-Membering Africa) Kugusia Kumbuhifadhi letu la kale katika Simulizi ya Jicho La Horus: Iliyotabiri Kutawalaliwa  na Kugawanywa Bara La Khemet. Lakini eti Bado analitumia Jina Africa. Mweusi kama unajitambua huwezi kutumia Jina Africa!

Si mwandishi pekee wa weusi ambaye hataki kutia nguvu zaidi katika  kuusema ukweli kama ulivyo, wengi tu kama yeye, ikiwa pamoja na wasanii,, viongozi na wataaluma. Wanashughulika na Agenda ya Usasa: post modernism badala ya ile ya Ukale: Ama classical antiquity

Kimat7

Dedan Kimathi: Kiongozi wa Maumau aliye uawa na Waingereza

Mau mau walisimama kupinga Ukoloni wa Mwingereza na kila kitu chake: Elimu , Dini na utamaduni. Kwa Maumau Mungu alikuwa anaishi kwenye Mlima Kenya. Ndio Nyumbani Kwake! Mau mau ulikuwa mfano wa kuigwa na Weusi wote. Japo kuwa walishindwa na kuuliwa, lakini waliunda na kuthibitisha hoja yao. Tanzania Chini ya Chifu Mirambo pia walifanya kama ndugu zao hawa. Warugaruga au watetezi na sio waasi, walikua maguerila waeusi waliosimama kupinga utawala wa kigeni. LEO WATU KAMA HAWA WANA JINA JIPYA WANAITWA MAGAIDI. Lakini wote wana hoja moja ya msingi inayofanana, kwamba iwe ya ,kidini  kitamaduni au kisiasa, wanapinga kudhulumiwa.

Hivyo kusema Bob:  Marasta na watu wengi wengine wampendao ni Bandia! Kanisa Katoliki lilifurahia kazi ya Bob na Rasta. Kwani hakuwapinga bali kuwathibitisha na kuwatetea: Vivyo hivyo WAYAHUDI. Mwishowe pengine walimuua asije kujitambua: nani ajuaye kwamba Vatican waliagiza kifo chake? Kwani wamewauwa wangapi?

Kila ukiwa na mvuto na kusikiwa na wengi, ukisimama hadharani kukemea Dini hizi za Ukristo na Uislamu, unauliwa!

lennon

 John Lennon

Mwanamapinduzi mweupe aliyewataka watu watoke katika dini na kuishi tu maisha ya upendo. Ukombozi wa mweusi ni ukombozi wa Dunia, ambayo watu wameifikisha hapa leo kwa mafundisho wanayodai ni ya Mungu lakini yamefanana na Ya kishetani Zaidi. Alichokisema Bwana huyu si Zaidi ya kuwaomba watu warudie MAAT Ile falsafa  Kongwe ya haki na Upendo ya Kikhemet. Katika wimbo wake wa Imagine ameliomba hilo. Lakini aliposema sisi ni maarufu kuliko Yesu kwa maana ya yeye na Bendi yake , na Pia kusema Ukristo utakuja kushindwa. Hapo maisha yake yalifupika.

Ukweli ni bidhaa adimu siku hizi, wahenga waliufahamu: ukweli ndio Mungu, na ukiukaribia tu, pia na kifo hakiko mbali!!! Wachache tu wamesalimika kwa na kwa nguvu za Lihumbile ( creation forces- nguvu za Uumbaji) kama Fidel Castro’

 The Church Committee stated that it substantiated eight attempts by the CIA to assassinate Fidel Castro in 1960-1965[10] 

MWISHOWE Bob akaonyesha rangi zake Halisi , alijifanya kinyonga lakini hatimaye akaumbuliwa na Waumbile( Miungu), Tamaa ya mali, ulafi na umaarufu, kama damu yake na babu zake weupe. Ungewezaje kumdharau Peter Tosh: Mwanzilishi wa Bendi ya The Wailers? Kirahisi hivyo? Bob aliicheza karata yake ya mwisho ya damu nyeupe. Na inavyoonekana alishinda lakini haku: Alikufa kwa huzuni, usiichezee mioyo ya watu uliowadhulumu. Wengi hawajui kuhusu kifo chake lakini namna ya pigo la adhabu lile. 

Sasa tunakuja katika kipengele cha mwisho, Bob Marley hakuwa Rasta kwa maana ya Mkhemet! Bob MARLEY HAKUZIKWA KAMA Rasta. Wangapi  mwalijua hilo? Tazama filamu ya Maisha yake : Bob Marley alizikwa Kama mkristo wa Ethiopian Coptic Church. Kabla ya Kufa kwake walimbatiza na Jina: Eti Berhane Sellassie. Makuhani wa hilo Kanisa walimfanyia ibada yake ya wafu.. So what is Rasta? Wewe ukijiita Rasta leo huna imani kwani Nabii wako Bob MARLEY ALIZIKWA MKRISTO. Mpweke, akijutia unafiki na usaliti wake, lakini akiwa na amali nyingi walizompa hao wachawi wenzie. Ilikua kama Musa vile, unabii ukijirudia: hutaiona nchi ya ahadi, kwani umetenda dhambi…..!!![11] Kifo cha Musa:

Ndipo Musa akapanda Mlima Nebo kutoka viinukao vya Moab mpaka vilele vya Pisga kupitia Jeriko. Hapo Mungu akamwonyesha nchi yote— KuTOKA Galielea mpaka Dani Naftali yotet na urithi wa Ephrahim na Manase, Nchi yote ya Yuda mbali mpaka BahriYa Mediterania, Pale Negebu nan chi yote ya Nagebu mpaka bonde  lote la Jericho na mji wa mitende, mpaka Zoaroar.  Na Bwana akamwabia: Hii ndio Nchi niliyokuapia kwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo Niliposema nitawapa warithi wako.’  Nimekuruhusu utazame kwa macho yako lakini hutaikanyaga”

Bob Marley hakuwa Rasta, kwa hivyo Rasta ni kitu gani ? Si lolote zaidi ya Tengenezo jingine kama Uislamu na Ukristo ambavyo vilipoteza mashiko yake kwenye Judism. RASTA  KATIKA ASILI YAKE ni  Ibada ya weusi, wala hawana shirika na weupe ifahamike hivyo. Biblia ni kitabu cha mafumbo, fumbo la Musa ukweli wake tuufunue. Eti mweusi hana Imani mpaka itokayo kwa wayahudi??/ Hapana, hapana hapanaaa: .Wayahudi walijifunza Imani kutoka kwetu.

THE BIBLE/ BIBLIA kama ilivyo QURAN

Kama viwayo vyote vile si lolote Zaidi ya  yafuatayo:

Yaani mafumbo ya kwanza (Agano la kale) na Mafumbo ya pili( Agano Jipya)

i.Kitabu cha fasihi iliyo andikwa kwa umahiri mno, ii. Kitabu cha mafumbo siri kuhusu ukweli iii..Mkusanyiko wa uongo uliobobea!

Aidha ikumbukwe kuwa QURANI NI MWAKISO TU WA VITABU VYA Musa.

Imani ya weusi Bob Marley akaifanyia Biashara, akaiuza kwa shetani kujipatia ujira wa damu, kama vipande 12 vya dhahabu alivyolipwa Yuda kumsaliti Yeshua. Lakini pesa hiyo dhalimu itatwatokea puani!Sio wayahudi, na hekaya yao kule Khemet ya Kishetani, wa Mungu ni watu weusi, na ambao ukombozi wao umekaribia sasa, watakusanyika na kurudi katika Nchi yao Kipenzi: TAMER

MAREJEO:

[1] The BOOK OF THE DEAD: Lost copies

[2] Mwaikoma 2014, BOB Marley : A critical Analysis

[3] http://www.dailymail.co.uk/news/article-2839424/This-dreamed-Family-Bob-Marley-launch-global-marijuana-brand-honor-reggae-king-cannabis-industry-braces-hit-10-billion.html

[4] http://www.ynetnews.com/articles/0,7340,L-4093267,00.html

[5] Neno la Kibantu likiwa na maana sawa na Guerilla au mwasi mpiganaji wa msituni

[6] Mwaikoma 2013: Of Music and Protest

[8] Allen, James P.Middle Egyptian – An Introduction to the Language and Culture of Hieroglyphs, first edition, Cambridge University Press, 2000

[9][9] Mwaikoma: A Contribution to the Critique of Religion: 2013

[10] Kumbukumbu la Torati 34 New International Version (NIV)

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s