RAISI KIONGOZI

ANDIKO LA MWONGOZO

G. A. MWAIKOMA

Miongoni mwa watu weusi Kiongozi maana yake ni Pharao’ Na huu ndio mrejesho na kielelezo cha  Kiongozi duniani mpaka leo, ‘ukikumbuka kuwa kumbu-hifadhi ya kale Zaidi duniani ni ya Wa Khemet’[1]

PHARAO1

PHARAOH: Asili ya Watu weusi na  Kielelezo cha Utawala  na wenye Mamlaka Duniani

UTANGULIZI

Cha Kwanza kabisa Raisi wa Nchi yoyote katika bara Khemet lazima atambue uhusiano wa kumbu-hifadhi la bara lake na hali ya bara hilo leo kwa ujumla wake. Aliye kutawala, kukuua, kukupeleka utumwani, kuua ustarabu wako, kufuta Historia ya Babu zako, kuchukua rasilimali zako nyingi, kukulemaza kiuchumi, hawezi kukuita jina! Akikuita jina ukalikubali unakiri, kukubali yote aliyokutenda. Zaidi kuafiki kwamba ni sahihi! Nawe utaendelea kujenga msingi wake kwa manufaa yake  wala si watu wako. Tu kwa sababu ya kukushinda kivita:Hawezi kufuta na utu wako wote Kabisa! Kwa hivyo kwa Ushindi wake kijana Alexander anaita kituo cha ustaarabu wa bara la watu weusi Egypt! Anapuuza jina la asili la Nchi hiyo ‘Khemet, anapuuza lugha ya watu hao ki Khemet, anachomekeza lugha yake na kulazimisha ustaarabu wake’ kwa mkono wakulia, kwa wakushoto anachukua maarifa ya watu hawa, falsafa, sayansi , hesabu, ujenzi, matibabu, Imani ya Mulungu na miungu. Wakati wao wanadai na kutetea hifadhi yao wa kwao dhidi ya wa  kwetu . Je Raisi Kiongozi anakaa tu Kimya? Ikumbukwe kwamba kulikuwepo kumbu hifadhi kabla ya hii tunayoiita Historia leo ( Hasa ya mseto wa wagiriki, warumi, waarabu na wazo la Magharibi kuanzia karni ya 17)[2] Raisi Kiongozi Lazima ahusianishe utu wake na Babu zake wa Kale, kupigania na kutetea hili kwa machozi , jasho na damu ikibidi.

Katika hayo hakika hatuta sahau ustaarabu wa Kiislamu kwa mchango wake katika kumbu hifadhi utamaduni na hasa Ibn –Khaldun ama baba wa hiyo[3] na Jitabu lake adhimu la Al Mukhadima au utangulizi wa Kumbu-Hifadhi. Sasa Raisi kiongozi lazima aanzie hapo. Pili Lugha asili lazima zipewe nafasi kubwa Zaidi katika ujenzi wa lahaja ya Taifa. Kama sisi watanzania tunayo nasibu kubwa kupitia lugha ya Kiswahili. Tatizo naona lugha asili zinapewa nafasi ndogo. Wengi wetu hatuoni fahari tukiongea Kiswahili pasipo kuweka aghlabu, mathalani, nusura,Raisi nk.’ Haya ni maneno ya kiarabu. Au protokali, agenda, birthday ,automatic( hata siku yakuzaliwa yatushinda kutamka! )Sio kosa letu, tumepata taarifa katika mizizi ya mfumo wa hao wageni. Mpaka akisha enda Ulaya mtu, akiwa muislamu au mkristo ndio utu wake umekamilika’ hahahahha! Sio makosa yetu, ndugu hawa waliotupeleka utumwani walitulazimisha kufanya hivyo. Lugha ni utaratibu, ukiitumia unajiratibisha ndani yake bila kupenda ! Pia kuafiki matendo ya aliyekupa. Athari yake ndio hii mpaka leo. Lugha ni ujuzi mtakatifu..walisema makuhani wakufunzi wa Khemet ya Zamani. Kwa kumsaidia Raisi kiongozi atambue na kuwajibika katika ukweli kwamba Dunia yetu leo kwa ujumla wake imekuwa na Kumbu hifadhi tatu: Ya Mweusi kama kongwe zaidi, ya Mrumi, Mgiriki na ile ya Mwarabu. * ukiiweka kando ile ya mchina..ambapo warumi na jeuri yao yote walichemka ..tena walikuwa mabwana wadogo tu..kwa Uchina! Leo hizo ndio lugha za msingi za kitaaluma duniani, hizo mbili za awali zikiwa Mama wa Kiingereza ambayo ndio lugha mashuhuri kuliko zote Duniani! Kwa hivyo utakuta katika Taaluma, msingi wa marejeo unakuwa Kilatini na kigiriki. Lakini kile kikemeti cha zamani, kilichowafunza ndugu hawa, kimefutwa. Sio masihara, kanisa la Romani liliwaua wengi makuhani wa Khemet miamba ya ujuzi na maarifa ya zamani, walionusurika wakakimbia na kujificha na ujuzi wao. Lakini hiyo ni Baada ya kuiba maarifa ya kutosha, yaliyo baki waketengeneza taaluma waliyoiita Egyptology eti utafiti wa ustarabu wa zamani wa Egypt, neno lenyewe Egypt ni makosa ya matamshi ya Kigiriki,  Asili Mji uliitwa Haweti Kapti. Wao kwa kushindwa kutamka, na kudharau kujifunza wakatamka Aeguptos na kwa makosa wakaiita nchi yote. Wakemeti waliita Lugha yao Medewi Neteri[4] Au kama nilivyoshasema tayari maneno matakatifu na mji wao Khemet au nchi nyeusi. Sasa unashangaa, kwanini hakuna Romanology na Greecology?  Warumi nao wakaendeleza mwendo ule ule na kuliita bara Africa, kutoka neno la Kikhemeti Afr  lililomanisha chemka au kuchemka! Kwa Jua kali na Joto walilolikuta kule! Kupunguza ustaarabu wa mtu mpaka kuwa somo lakuchunguzika! Sasa Kwa Raisi wangu Kiongozi lazima uyathamini haya! Asili ya Babu zetu na rangi yao ya mwili limekuwa jambo la kubishaniwa katika harakati za kutunyang’anya urithi wetu. Kwa nini masanamu ya wakhemeti hayakuwa meupe kwa kujengwa na Marumaru? Bali majengo yao mengi na masanamu walitumia rangi ya udongo na udongo wenyewe, shaba na chuma, wakipaka rangi nyeusi? Wao mbona masanamu yao ni meupe? Haifichiki kabisa , katika kumbu-hifadhi ya zamani kumekuwa na watu watatu duniani, mweusi wa kale kabisa, wa mashariki, na wamagharibi,  ambae ni mzazi wa Hawa wazungu wa leo ama Wa Aryani! watu wa Kaskazini. kila mmoja akiwa na sehemu yake mahsusi kabisa kijiographia, inayombainisha, mweusi ni wa kusini mwa tufe: bara na ustaarabu wake wa Khemet. Katika kitabu cha Hekalu La Khemet waandishi wameyasema haya kwa kina na ubaga. Ile inaitwa jadi na asili, wao wakaita upagani ndio msingi wa ustaarabu wote na wa dunia. Na kama wetu ni upagani wao ni upagani ulionakshiwa. Raisi Kiongozi pamoja na kutoa kipaumbele kwa Lugha za asili kuchangia kwa upana Lugha ya Taifa pia aruhusu ibada ya imani za jadi , itakayo boreshwa kukidhi mahitaji ya sasa. Na huyo mganga wa Kienyeji asidharauliwe bali awezeshwe. Kama zilivyokuwa Imani za kidini, matibabu ya kisasa yana deni kubwa kwa waganga wa kienyeji. Katika kumbu hifadhi ya Kale hawa ndio walikuwa makuhani waliobobea katika maarifa. Raisi asiishie kwenda kwa waganga na mafundi kifichu fichu. Awape heshma yao.  Mfumo mzima wa Elimu uyazingatie haya. Kuanzia hapa sasa akishayajua haya Raisi kiongozi, Jiji la Dar es Salaam lirudie jina lake la asili la Mzizima. Mwarabu na dini yake, tunamuheshimu sana, lakini alitukuta hapa na mambo yetu. Na sio tu hapo, tuite miji, mashule, majengo, barabara , sehemu na vituo vingine kwa majina ya Wahenga wetu. Hivyo zile Baraka na asili yetu zitaturudia. Na hatimaye tutaikomboa Khemet nzima. Si tu pale Misri! Kituo cha Mamlaka ya Bara la weusi cha Magharibi. Waakawapa waarabu Manomadi wajangwani wale, na kuitumia dini ya Kiislamu na Ukristo kutugawanya na kututenganisha. Asili ya Ukristo na Imani nyingi karibu zote zingine ni Sisi hapa.Tembea makaburi yote uangalie, utaiona mingi misalaba, je unajua maana yake? Ni Ule ufunguo wa Khemet, ishara siri ya Khemet au ANKH[5] , Dhana iliyoibwa na Warumi nakutengeneza dini ya Kikristo wakichanganya upagani wao, imani jadi za mababu zetu na Imani za kiyahudi. Musa Mwanzilishi wa Imani ya Juddism na mkumbu hifadhisha wa kwanza mgeni wa kumbu hifadhi ya Babu zetu alikulia Khemet, kwenye jumba la mfalme, akiandaliwa kuwa Farao, akajifunza mambo mengi mno. Wayahudi hao wana wa Israeli wanaingia Khemet kama Manomadi wachunga kondoo wa nyikani, wanatoka wakiwa wamestaarabika, wamejifunza Lugha yao hiyo, kuandika, hesabu , kuweka kumbukumbu, mpaka Sanaa ya maziko kama inavyothibitika katika Biblia. Khemet Lilikuwa jiji Mashuhuri la kale. Leo ilikuwa kama ilivyo kwetu kwenda Ulaya. Wengi wetu tuna amini maisha mazuri ya Ustaarabu, taratibu na Demokrasia yako Ulaya. Hivyo ndivyo Ilivyokuwa Khemet ya zamani. Mataifa yalipogombana walitafuta suluhu, ama mkono wa ulinzi Khemet. Na walitoa ushuru kwake. Yesu huyo mtu mashuhuri kabisa katika Ukristo alikulia Khemet. Yeye amekaa Uyahudi mara mbili tu : Kwanza baada ya kuzaliwa, pili aliporudi amekamilika kufanya kazi yake, miaka mitatu tu, na akauliwa na WARUMI. Je hicho kipindi chote cha katikati alikuwa wapi, akiifanya nini? Khemet; Nchi ya Amani , salama ya makimbilio. Na tunajua katika maandiko ya Kale ya Khemet Yesu kwa Maana ya Assar alikuwa ametabiriwa. Na Judism ndio Baba ya Uislamu. Muhamadi anasoma vitabu vya Musa kwa msaada wa Wayahudi walioishi Arabia, anaanzisha Imani yake ya Kiislamu. AMBAYO IMEFANANA SANA NA Judism isipokuwa Machache tu! Nikisema ukristo ni upagani tusigombane. TAFUTA ASILI YAKE ULIKOANZIA. Ndio sababu mi nafurahi kuitwa mpagani, kwani kama iko imani yeyote ile nyingine, isiyoupagani, basi nionyeshe nitaifuata. Wewe ukiweka sanamu lako hapo wanakuita mpagani, kwao wameyajaza, lakini hawakwambii maana yake: ni walinzi na kumbukumbu ya ustaarabu wao (The Guardians) Wale pale sio kwao, ndio sababu asili, mila, desturi zao hazifanani na wale Babu zetu wa Khemet ya zamani. Wakijifanya kuhifadhi kumbukumbu za kale kumbe wanazifuta kimfumo ujanja! Wasomi wetu nao pamoja na majukumu yao yote mengine, kipaumbele waweke katika hili, katika kutafiti, kuibua na hatimaye kuunganisha hifadhi kumbu letu la kale na utu wetu wa leo. Raisi kiongozi awe Raisi wa watu, awe karibu na watu wake kwa kupitia haya. Wasomi wawakumbushe watoto utu wao wa kale, wasiendeleze kazi ya kuifuta. Kama mamluki. Raisi kiongozi ajikite katika kujenga Taifa zuri, kwa kutoa kipaumbele kwa upatikanaji wa huduma jamii bora zote mpaka vijijini. Na kuziitupilia mbali falsafa uchumi mbovu za udubwana miji (City Bourgeoisie) . Raisi afuatilie kila senti na shilingi imetumika kwa makusudi yake katika kujenga shule na upatikanaji wa Taarifa Bora. Miji ijengwe katika misingi ya ujenzi unaoibua taswira za asili yetu, kama babu zetu kwa masanamu na kumbukumbu za watu na matukio mashuhuri. Tusiishi kuishia kumbu hifadhi ya kisasa(Modern history) bali tuunganishwe na ile ya kati( Medieval,na ya kale:Ancient History) Daima nguzo kuu za msingi ni Tatu Babu zetu wakilijua hilo wakasimamisha mapiramidi yale, na Maegyptologist wanapuyanga lakini katu hawazing’amui siri za wazee wetu wale. Mabingwa wa Ishara na michoro ya kisiri (Mysteries and codes) au wanajua lakini wanaficha kwa makusudi. Raisi kiongozi awe mtu wa watu, ajenge nguvu yake kwa kuwapenda hawa watu na kuwafanyia mambo mema. Kuwe na Mabustani, watu wakapumzika na familia zao na wapenzi wao wakifurahia na kuipenda nchi yao, kwani nchi imewapenda wao kwanza, kwa neema zote na rasilimali, kwa nini ziwafaidishe wageni! Kwako wao wenyeji ‘kwao wao we mgeni,, hii inakuweje? Maktaba bora Zaidi ziongezwe na watoto wakumbushwe asili ya maandishi na vitabuni ni yao na bara lao, wala wao sio manyang’au bali baba wa ustaarabu. Tunapenda Amani lakini tutapigana kulinda utu na asili yetu. Ndio Raisi Kiongozi awe mtu mnyoofu kabisa. Biblia imethibitisha Mafarao walikuwa watu amini na wanyoofu.

Na Mungu akamwambia katika ndoto, ‘ Ndio najua ulifanya hivi kwa Uaminifu na unyoofu wa Moyo wako. Kwa hivyo hata mimi pia nikakuzuia usije nitenda dhambi’ Hivyo sikukuruhusu umguse’[6]

Nukuu ya Biblia katika kisa ambapo Farao alimpenda Sara Mke Wa Ibrahimu, Ibrahimu akihofia kuuawa anamdanganya Farao kwamba Sara ni Dada yake. Sio Kama msemo wa Waislamu eti ukiyastaajabu ya Musa utayaona ya Firauni, Farao walikuwa Viongozi adhimu na rahimu. Kilichowakuta Wayahudi ilikuwa ajali kazini. Wewe Kiongozi unalinda maslahi ya watu wako. Wakija watu miongoni mwako, wanazaana wanaingia kila mahali, utapata hofu ya kiusalama. Utajaribu kulitatua suala hilo. Ndivyo alivyofanya Farao yule. Lakini Hatuwezi kubatilisha mema yote kwa mabaya machache. Na hili liwe fundisho kwa viongozi wa leo Khemet!

Raisi Kiongozi onyesha mfano wa kuthamini asili yako, kwa kuthamini utamaduni mila na desturi. Japo Hata Mara moja Raisi Kiongozi vaa Mavazi ya Asili uwakumbuke Babu zako. Sio Raisi unagonga suti kuanzia mwanzo wa utawala wako mpaka mwisho! Eeh..heheh, Japo hata mara moja Shekhe! Sasa eti linatafutwa vazi La asili, umekuwa mradi, hata sijui umepotelea wapi! Mavazi tunayajua, ni kuvaa…Badala ya kuhudhuria hizo hafla za Binti Tanzania, mabinti wakivaa mavazi na vichupi vya Magharibi. Sisi tuna namna na mavazi yetu tele. Tazama michoro ya zamani ya wakemeti, wakati majirani zao hao wakiishi kama wanyama Wakhemet walikuwa wanavaa mavazi mazuri, na vito vya thamani.

nyerere asili

Mwalimu Nyerere Maramoja moja aliheshimu mavazi ya Jadi

Mwisho kabisa Raisi kiongozi wangu wewe ni Farao Jitambue unabeba si tu nchi, na roho za watu, wewe ni Kama Mungu au Mwakilishi wake kwao, unadhamana. Basi Ukawe na mpenda haki, mwaminifu, usipende udhalimu, Rushwa ikatae kabisa, ona ilikotufikisha leo.  Ukawe na nidhamu ya Kijeshi. Ukiisha kuhakikisha unyoofu wako, basi usiogope kuadhibu, hata kwa adhabu ya kifo. Kwa wadharau maonyo na wakiuka  maadili! Mwalimu wala mkufunzi hawezi kulala na mwanafunzi, wala mtu kumbaka mtoto. Toa adhabu kali, tena hadharani, Taifa zima lione, wajue tunaongozwa kwa misingi ya haki. Mbele ya sheria hakuna lele Mama. Tena ukaadhibu kwa Haki. Hawezi kuuliwa mwizi wa mbuzi na wananchi, mwizi wa pesa za kusaidia Hospitali ya wakina Mama akaachiwa tu hivi huru, eti unambadilisha Ofisi, hiyo ni dhambi na itakuchafua. Watu wakilalamikia hukumu yao inakuchafua. Asante sana Farao Wangu

Wako mwaminifu Kwa Ujenzi wa Khemet

G. A. MWAIKOMA.

Aidha RAISI KIONGOZI: MWONGOZO

Muswaada uko katika hatua za awali. Ukikamilika tutaarifiana. Raisi wangu usikose kukisoma kitabu ukawa Kiongozi mwema na adili kama Babu zako

[1]  “The Cuneiform Writing System in Ancient Mesopotamia: Emergence and Evolution”. EDSITEment. Retrieved 16 December 2013.

[2]  Ibn Khaldun, Franz Rosenthal, N. J. Dawood (1967), The Muqaddimah: An Introduction to History, p. x, Princeton University PressISBN 0-691-01754-9.

Ibid 2. Kott, Ruth E. “The origins of writing”. The University of Chicago Magazine. Retrieved 16 December 2013

[3]  Dr. S. W. Akhtar (1997). “The Islamic Concept of Knowledge”, Al-Tawhid: A Quarterly Journal of Islamic Thought & Culture 12 (3).

[4]  Carruthers, 1994, University of Sankore Press.

[5]  Collier, Mark and Manley, Bill. How to Read Egyptian Hieroglyphs: Revised Edition pg 23. Berkeley: University of California Press, 1998.

Ibid.  Inman, ThomasAncient Pagan and Modern Christian Symbolism, Second Edition. New York: J. W. Bouton, 706 Broadway. Published 1875. Page 44

[6] Genesis 20:6)

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s