G. A. Mwaikoma

A.K.A  Kina  Gah Ubaagah

Noveno de Octubre 2014

gueva1

Leo tena msituni, kule La Paz Bolivia. Hatumkumbuki aliyekufa, si kitu, isistoshe siye wote marehemu watarajiwa!Ni namna utakavyo ondoka.  Kwa heshma au Aibu! Mawili hayo inategemea na kile ulichochangia katika zoezi zima la uumbaji linaloendelea. Imesemekana kwamba Mungu hakukamilisha kazi yake! Kwamba aliumba miili tu. Jukumu la kuumba Roho akatuachia. Sio muhubiri mimi! Tuko pamoja’ Uumbaji wenyewe ni katika mahusisho jamii! Yaani tunavyo shirikishana katika ya kila siku. Uumbaji wenyewe ni katika kufikia ile ndoto ya aina binadamu kwenye tufe ya dunia: Wanao heshimiana na kuongozwa kwa misingi ya haki na upendo. Hii bila kujali rangi zao, dini, itikadi n.k

gueva2

Kwa ajili ya dini tunachinjana kila siku. Kwa namna moja ama nyingine Dini zimetuangusha. Harakati hii ni harakati kombozi katika wakati wa sasa! Binadamu kokote alipo asiteseka bure tu! Na wakati utatuzi wa wanayo mkabili upo! Isipokuwa wakina fulani tu kwa sababu ya wendawazimu wao’ basi wameamua ‘hali mtu hapa leo hadi nirudi! Kurudi penyewe hawarudi, wanapumzika kwenye malalo yao, siye twapiga miayo tukiwangojea, waje kutupa chakula cha leo, sio makombo na mizoga ya jana. Makubwa hayo..lakini binadamu tusifanyiane hivyo! Sasa kama wewe mgumu kama chuma, basi maji na hewa ya mapinduzi vitakutia kutu na kukurarua kabisa.

gueva 5

Leo Ndio tunamkumbuka Che katika hilo. Mapinduzi ya leo ni ya kitaarifa zaidi. Watu wakajitambue wao ni nani na ni nini nafasi yako katika ujenzi wa tufe bora Ya Dunia, sio buree! Sio Lazima Bunduki. Tusiwe shingo ngumu mmpaka tufikishane huko. Tusiuane tu kwa sababu tumeshika au tunaweza kupata silaha. Tusitafute ugomvi sababu tuna biashara ya silaha! Au sababu tuna Mafuta tunaweza kuzinunua! Rasilimali zitumike kwa maendeleo bora ya jamii.Tusiwalazimishe watu utashi wao wa ibada! Alokwambia we miye nimepotea hajui huyo huyo alomuumba yeye ndo kaniumba miye? Au wako wawili! Wakisha kuwa wawili basi maana yake haipo..yaani kwa maana nyingine hata mwenyewe hayupo kabisa..na uhai ni umbwe tupu: tabura rasia. Zingine nazo’ hivi kweli ni imani na itikadi au upagani mambo leo? Tena hata huo upagani tuuacheni, kwani ni bora kuliko huu wendawazimu wa leo. Yaani we ukamchinje mwenzio eti thawabu kwa Mungu wako? Huyo Mungu gani? Ukamchome moto! Bora miye mpagani, tena mpagani kindakindaki, nashikilia imani ya babu zangu ya zamani. Imani ya upendo na jadi. Lakini moja nikukumbusheni ‘ huu upagani wangu ndio Mama wa hizo dini zenu za leo!

Che Guevara Leo kwa ajili ya hakielimu, haki rasilimali haki ulinzi na usalama, na haki uhuru wa ibada, kama mwaishi kwetu kwa amani kwa nini kwenu hamtutaki? KWENU MWACHINJANA na wale wenye kuwapokeeni wakawastirini tena wamekuwa wabaya! We mi nimekukuaribisha kwangu! umenikuta na ya kwangu! Ghafla wataka kunibadilisha tena nifate yako! Yalokushinda huko kwako umekuja kwangu hapa! Nyie waja vipi! Watu walipigana ilikuwakomboa wenzao kwenye makucha ya unyonyaji yalo tu shika hata leo, , wengine wataka kutuleta wazimu wa vita kwa ajili ya dini? Ok sasa kama mimi siyo dini yako ukishinda vita unichinjeeeh? Wacheni ujinga’ Binadamu wote ni kiumbe kimoja! Amri ya Mwisho Upendo.Ikishindikana hii itategemea nani anadhulumiwa. Na hapo basi tutapigana! Wala hatuogopi kufanya hivyo itapobidi!

gueva3

Hasta la victoria Siempre!

Ernesto De La Serna Guevara

Nacido: 14 de junio de 1928, Rosario, Argentina
Murió: 9 de octubre de 1967, La Higuera, Bolivia

Real revolutionaries adorn themselves on the inside, not on the surface.

  • As quoted in Che Guevara: A Revolutionary Life (2010) by John Lee Anderson, p. 178
 • We cannot be sure of having something to live for unless we are willing to die for it.
  • As quoted in Wise Guys : Brilliant Thoughts and Big Talk from Real Men(2005) by Allan Zullo, p. 36
  • Asanteni Sana
  • Aidha usikose kukisoma kitabu cha Mwaikoma:”  Hekalu La Mulungu” kitakachotoka  mwezi April mwakani, ambapo amedai upagani ndio msingi wa imani na dini za kisasa, yaani upagani ndio msingi wa ustaarabu wa jamii binadamu wa leo, kila anachokifanya binadamu anajifunua tu asili yake na kule alikotoka. Changamoto kali kwa wana sayansi jamii na Falsafa
  • * Fyale Waya: Mwana Wasifu na Mhakiki wa Mwaikoma
Advertisements

2 thoughts on “KUMBU KUMBU LA III LA CHE GUEVARA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s