MKONO UKICHAFUKA

SEHEMU YA II

(AMA: VISA VYA WAKUNGA)

NA G. A. MWAIKOMA

JAKAYA1

JAKAYA KIKWETE AWAMU YA NNE

A.K.A VASCO DA GAMA, MZEE WA ZIARA A.K.A MZEE WA VIPUSA na Serikali ya kishkaji!

Kuwa wazi tu na mkweli: kura yangu mi sikumpigia. Sasa kabakiza mwaka wake mmoja ajondokee zake na mali zake, atuwachie watangaa na nyika ufukura wetu, kwani tushauzoea ulofa wetu . Uzuri wetu Wazaramo hatuna hiyana wala ubaya na mtu, kero yetu ukweli’ huo lazima tutakwambia. Ikishindikana kabisa basi kwenye Mdundiko  kama ilivyo sindimba kwa wamakonde, taarabu  na madufu! Kamailivyo wahi kusemwa  mdundikoni: Baba kavaa suti’ Lakini kaputura ya Mwanae inamiwani makalioni!Tulikuwa chuo kikuu pale mwaka huo 2005, kijana kama walivyomwita akaja kupiga kampeni. Lakini mi haikuniingia akilini, huyu mwaka 95 ye na rafikiye Lowasa AKA Boyz II Men waliambiwa na Nyerere “Kampeni mwapiga na buibui Ulaya hilo, pesa ni wapi mlikozitoa? “Yakaja yakapita kama tulivyokwisha zoea kupumbazwa na ulofa wetu. Katika utawala wake tumeshuhudia kufichuka kwa tuhuma chafu kabisa ya Serikali ya yule alomtangulia yaani Mkapa: EPA, na ile ya RICHMOND. Lakini hakuthubutu kumgusa Mkapa, na Sumaye, au ye mwenyewe kujiuzulu! kapiga piga chenga zake, muda ushapita anajiondokea zake. Yalianzia kwa bwana Mwinyi, yakaotea mizizi wakati wa Bwana Beni, sasa Kwa Da Gama kama dudu au nyama ume limekamilika, ikulu imegeuka kuwa jumba la wanyang,anyi! Angekuwa Mjeshi kweli kama waandishi wa shajara na wasifu wake wanavyomnadi angefanya uadilifu. Akavunja vunja vyombo huru vya serikali, ikiwa pamoja na mambo ya ndani, dola, bunge na usalama wa Taifa, kisha akatumia vyombo vya habari kuupindisha ukweli kadri ya matamanio yake, matokeo yake ni hali tete kabisa ya kigaidi Tanzania. Kudhoofika kwa usalama wa Taifa. Kaikojolea kambi alikolelewa…naye atafanya kama AlexFerguson wa Manchester United, kumtafuta Mscotish Mwenzie ampe timu, bila kujali hili ni Taifa huru la watu linalopaswa kuongozwa kwa misingi ya demokrasia na haki za binadamu katika karne hii ya 21. Mheshimiwa rekodi zako kwa wana habari aidha si safi sana, wengi wameteseka, kutobolewa macho, kuvunjwa vidole na kumwagiwa tindikali! Kisha unafunika kombe ukijifanya mwana michezo! Mara kipenzi cha wasanii. Ukafungua studio, ukawapa washkaji zako,kwa hivyo kuna ubaguzi miongoni mwa wasanii. Lakini wenye macho yetu tunajua na kukumbuka vizuri sakata lako na wakina Mwanzo Mpango wasanii kutoka Kongo ulowatia ndani katika mazingira ya kutatanisha. Kifo Cha Mwaikusa, Mvungi. Na yale masahibu yalowakuta wakina Mwakyusa kwenda kutibiwa India. Ya Mungu mengi bwana tunashkuru bado wako hai.Tunachotaka kukwambia wewe nawe muheshimiwa ni tone tu katika bahari, binadamu si mkubwa kuliko nchi na mbingu. Hii nchi we uliikuta , na utaiacha, jenga jina na heshma yako kwa kutenda haki. Badala ya kuwa mwana mapinduzi wa haki, Dagama ametumia jeshi kuzimisha harakati za haki na kweli. Kama Mtwara pale, badala ya kukabiliana na wananchi ana kwa ana, au kwa hotuba maridhawa, unatuma jeshi kupiga na kuua. Mkuu wa majeshi Mwamunyange ameshindwa kumkatalia palipo maamuzi mabovu Raisi wake mwenye mamlaka Lukuki ikiwa ni pamoja na Ukuu wa Majeshi. Mwanajeshi  kutesa wananchi wako badala ya kuwa Komanda wa watu kama wakina Che Guevara na Fidel Castro.

Camilo Cienfuegos y Fidel Castro 1959

Castro na Camillo Mapinduzi ya Kyuba July mwaka 1959 bado yamesimamisha mfano wenye hamasa kwa wapenda haki duniani

Mheshimiwa akasaliti kabisa ndoto ya uzalendo ya Nyerere. Bali utawala wake umeungana kabisa na mabeberu kwa mikataba ya kishetania iliyo na inayowezesha rasilimali za hili Taifa kufyonzwa na wageni.  Sasa katika uharamia wa pembe za ndovu na Faru ndio usiseme! Viumbe hawa maskini watapotea katika uso wa dunia sababu ya anasa za matycoon flani hivi kutoka Uchina na Arabuni. Tunafahamu waheshimiwa nao wanakamisheni zao! Ndio sababu Jeshi liliposema liingilie kati, Bunge likapinga! Rushwa hata iwe ya aina gani inaanzia ikulu, kama nyoka piga kichwani. Akiwa Mwadilifu Raisi we na mimi mtu baki tutafanya nini? Asante sana mheshimiwa twakutakia maisha mema baada ya kuondoka kwako. Na wale vibaraka wako wakina Mwamunyange wakumbuke, kukataa madaraka ili kutunza utu, kweli na haki si kosa la jinai.  Yule Mmarekani mswahili  Jenerali wakati wa vita vya Iraki Bwana Colin Powell alipoung’amua mchezo sheri wa Raisi wake Bush Mkubwa, alijiuzulu wadhifa wake  kama  Katibu wa Serikali ya Marekani. Kama nilivyokwisha wakemea wasomi wa Tanzania AKA WAZEE WA TITLES, NA KWAMBA MFUMO WA ELIMU YETU HAUJENGI KUTUKWAMUA, bali kutengeneza tabaka la wachache, wanaojifaidisha kwa utapiamlo wa taarifa kwa wenzao. Swali linakuja sasa machapisho yenu nyie wasomi wa Tanzania yako wapi, mbona hatuyapati maktabani, lini yatawafikia wananchi chini huku wakajua Bwana fulani na fulani ni wasomi adhimu wameandika kadhaa wa kadhaa kuhusu hili au lile kwa ajili ya ujenzi wa Taifa? Wakisha itwa Profesa na Dokta( Na wengine wa kupewa) Kwisha kazi wanarudi maofisini kuendeleza wizi wao kwa kalamu na makaratasi, wanao adhibiwa wezi wa kuku na mkeka, wanawachoma moto.  Wacha nimalize andiko langu na kisa cha wakunga waliokuwa wakiwaua watoto sababu ya kuhofia miongoni mwao yuko mtawala wa kweli na wa haki kama walivyoagizwa na mfalme dhalimu aliewatawala binadamu. Siku moja mfalme wa Mbingu akakutana na Malkia wa nchi wakasema watu  katika nchi wamezidi kulalamika utawala mbaya wa binadamu wenzao. Kwa hivyo tumpeleke mwanetu aso zaliwa nao kwa sura kama mmoja wao akashinde vita awatawale kwa wema na  haki. Japo kuwa ilikuwa baada ya muda mrefu sana. Lakini hatimaye siku ikafika watu wakaamua kupigana kwa ajili ya haki zao, miongoni mwao kijana mwema akawaongoza mpaka wakashinda vita nakumwondoa yule dhalimu. baada ya vita alikuwa majeruhi, lakini akawaita mlimani vita ilikoshindiwa akawapa wosia kwamba watawale nchi kwa misingi ya upendo na haki. Kisha akawaambia yuko salama watangulie nchini kwao wakaitawale nchi naye atafuata. Walipokwisha ondoka kijana yule akachukuliwa na upepo na kupotea bila ya mtu kumwona. Wakunga watawaua watoto wee, watawala watarithisha watoto na marafiki zao  ufalme wao WEE!Lakini iko siku atakuja atakaye zaliwa na mbingu na nchi na huyo ataikomboa nchi ya babu zake na kuyatunza maagano.Asanteni sana.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s