luta

LUPITA NYONG’O

Kwa kweli wote Waafrika tumefurahi, kimaso maso Mwanangu msinirogeeni,, cherekooo! Ni Kenya tena…..Baada ya Mwanamke wa kwanza kutwaa tuzo ya Nobeli, sasa binti maridadi kabisa  kajitwalia Oscar. Filamu yenyewe ya MIAKA 12 UTUMWANI ya Mcqueen nayo nzuri tena yenye ujumbe adhimu. Wengi wamesahau utumwa. Hata kama wanakumbuka wanafanya nini kuuhusu? Sisi wapenda mapinduzi tunafurahi kwa ajili ya Kenya. Kenya kwa ajili ya Afrika. Rafiki yangu ameniambia jana jioni kulikuwa na filamu ya Waangari Maathai  pale kwenye Maktaba ya Marcus Garvey,Tottenham London. Maathai alifanya kazi nzuri kuikomboa jamii yake kupitia mradi wa kupanda miti.

Wangari-Maathai--007

Hayati Prof Waangari Maathai (R. I. P) Sasa huyu ndio miongoni mwa manabii wa Kiafrika kwa mtizamo wangu /Kama mshumaa gizani’ Waangari ameacha nuru kuu ambayo wapenda haki bara la Africa tutaifuata. Hakurudishwa nyuma wala kuyumbishwa na siasa chafu katika utawala wa Moi.

Ukiichunguza historia ya filamu ulimwenguni utaiona nafasi finyu ya mtu mweusi. Imesemwa kwamba filamu zilianzia Ulaya, au Magharibi. Filamu kwa maana ya ufundi. Lakini sasa staarabu zote duniani  wamefanya filamu zao. Wale wasioweza kabisa basi wanawakilishwa na wenzao. Lakini mwakilishi si muhusika halisi. Afrika tumeteseka mno kitaarifa kwa sababu ya uwakilishi. Akikuwakilisha mwingine basi hatekelezi kama utashi wako. Ni kama ilivyo hoja ya utafsiri. Basi waafrika bwana ni kama mtu aloomba aandikiwe wosia na mtu  aso mwaminifu. Kawanyima watoto urithi kajiandika yeye.

Sasa Lupita Nyong’o anatutia sisi wapenda Bara na Heshma ya mtu mweusi hamasa kuu. Lakini Lupita si hadithi ya Mashaka. Zaidi ya kupuuzwa fani ya sanaa katika utawala wa Moi tena. Maraisi wengi wa Africa wanaipuuza sanaa, na mara nyingi wamewatesa wasanii kwa sababu za kisiasa. 

Waheshimiwa wanapenda sana utukufu, basi wanatakakuwafanya wasanii ndege kasuku kuimba au kutoa kazi zaidi kuwatukuza wao. Wakati wa mambo hayo umekwisha pita, wasanii watambuliwe na kuheshimiwa kwa mchango wao katika ujenzi wa Taifa, na katika hii mada basi bara la Africa. Kwani msanii wa kweli yuko kwenye daraja ile ile ya kinabii kwa maana ya uongozi na ukombozi wa jamii yake. Baba mzazi wa Lupita ni Profesa Anyang Nyong’o. Lupita ametunukiwa kwani ametoka katika familia ya wanataaluma magwiji. Pengine hali hii imechangia kumjenga utu wake. Hii haimaanishi tuwe watoto wa maprofesa kwanza ndipo tupate tuzo. Si watoto wote wa maprofesa wamepata Tuzo ya Oscar. Mwenyewe Lupita kajipigia Shule yake safi tu. Ya kwanza pale Chuo Kikuu Cha Hampshire Marekani na kufuzu mambo ya Filamu na Sanaa za Jukwaa. Na kisha kuwa msaidizi wa utengenezaji wa filamu katika matengenezo mbalimbali. Kazi yake ya kwanza ikiwa East River ikifuatiwa na Tamthiliya ya Runinga ya Shuga, na kisha kuongoza filamu hifadhi ya IN MY GENES‘. Hakukomea hapo, Nyong’o akaenda tena kunyuka  shahda yake ya pili pale shule ya maigizo Yale.  Baada ndipo kushiriki kazi hii mashuhuri ya Bwana Mcqueen’ LAKINI NI UKWELI USIOPINGIKA KWAMBA TAALUMA INAKUONGEZEA WIGO WA FURSA. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kazi yenyewe ile ya 12 YEARS IN SLAVERY : NDIO‘ MSINGI WA MAFANIKIO YA LUPITA. Ni kama timu mzuri kupata mchezaji mzuri! Binafsi nimefurahi sababu tukipata wengi waafrika, katika medani hizo viwango vya kimataifa basi pia tutazidi kupata uwakilishi mzuri. Taarifa mbovu kuhusu bara la Afrika na Mtu mweusi zitaendelea kunyooshwa. Ni majuzi tu hapa waafrika wameanza kuwa washindi katika filamu za magharibi na mashariki. Mara nyingi ni watumishi au wahusika watovu.Mjaluo huyo, kala kapeti jekundu Hollywood na jina lake la asili. Mkono kwa mkono na Brad Pitt na Mkewe Angelina. DADA ZETU WANATAKA KUWA WEUPE: LUPITA KISIKI CHA MPINGO na bado kadundika mjengoni vile vile . Japo sijui dini yake. Hoja yangu ni kwamba wakati lazima ufike mwaafrika asiipuze utu na historia yake.  na vijana wengine wameamua kutafuta binti weupe tu! Lakini juzi nimeona  Binti wa kizungu kaacha maisha yake London pale anakwenda kuishi na Mmasai wake umasaini.. Tusilaumiane. Mazingira yalijengwa na hata sasa yapo yanayotufanya tujihisi waswahili sisi si watu wakamilifu. Lakini dhambi ya ubaguzi ilivyo bwana, walivyomaliza kutubagua sisi, wakaanza kubaguana wao kwa wao. Na wakina fulani walioachwa na mzungu wanatufanya sisi mbwa lakini ukienda kwao, kumbe watu tu kama sisi, tena hata wanamatatizo makubwa zaidi. Lakini wako kwetu hapa wamejichumia maisha mazuri bali wanatudharau siye kweli kweli! Lakini tutafika tu mazee. Hata kama kwa kutafuta uraia katika nchi hizo ziitwazo zimeendelea.

Kwani Lupita  ana uraia pacha, yaani Kenya na Mexico. No way lazima tujilipuwe mazee!

Kenya mi na wapenda, pamoja na matatizo yao ya kisiasa na tofauti za kikabila, wanajitutumua mtu binafsi binafsi mpaka wanaonyesha tofauti. Ukidhani wale wenye umoja watafanya ya maana zaidi’ wapi tunakenua meno tu…! Kama nilivyosema awali si fulani wala fulani, tufikirie bara la Afrika. Ngugi Wa Thiong’o mteteaji mkubwa kabisa wa mila na desturi za kiafrika amepata kusema, kwamba unapoindoa mila unauondoa na utu wa yule mtu. Kwamba tamaduni zina athiriana sawa, lakini kwa makubaliano maridhawa. Lakini tusipigane kupata tuzo Ulaya. Viongozi Waafrika wana subiri nini kuunganisha hili Bara? Tuwe na Tuzo zetu. Na kudumisha kipaumbele Historia , mila na desturi zetu ?

.Ngugi1

WaThiong’o

Kwa hivyo kwa waraka huu wapongezi na penda kutabaruku kwa ajili ya Waafrika wote waliokanyaga tufe hii ya Dunia kwani kila Mwafrika ni nyota Kuu.

lupita3

Pongezi sana Dada Lupita

Mwisho kabisa Historia isiwe kisingizio cha kuboronga. na hata kama ikiwa, ni muhali kuisahau biashara ile dhalimu ya utumwa.

Kwa sasa ni kumbukizi lake viza katika Siasa mbovu, miundo mbinu hovyo, na kunyimana taarifa kwa makusudi Afrika. Napenda kufanya nukuu hapa kutoka hadithi ya Bwana Sina jina:

Alo waambia ni nani? 

Mimi sina jina Jina langu ni nani? Hivi nyie mwalijua? Eti mmenipa jina

Mkaniita jina Mlipokuja hapa mlinikuta

Sina jina, Na jina langu mtalijua: Mimi nipo hapa

Sina jina

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s