MKONO UKICHAFUKA HAUKATWI
TANZANIA: KUKUBALI MAKOSA
Gamier Mwaikoma

10/Feb/2014

amigo3

The Three Amigos

Mkapa ,Mwinyi na Kikwete Kwa Pamoja wameshirikiana kuusaliti Umma wa  Tanzania Kwa kuikiuka misingi ya Taifa iliyowekwa na Mwalimu Nyerere NA MIONGONI MWAO watatu hawa na kabineti zao, rasilimali, malighafi na urithi wa Watanzania umegawanywa na kutapanywa!  bila ya aibu wala huruma! Na huyo wa tanoTwa msubiri akenda tezi na Omo kurejea ngamani! Atuanulie Tanga msibani’ 

Katika kitabu changu cha “Shule Mfano wa Taifa* ” Nimesisitiza kwamba si Tanzania pekee bali Africa inatatizo kubwa la kitaarifa kwa maana ya upatikanaji, matumizi na athari. Kimsingi tuna tatizo-Mama la Kitaarifa’ Menginewe matokeo.

Shule na Maktaba ni vyanzo vikuu viwili vya Taarifa. Taarifa ndio nyenzo kuu kabisa ya binadamu zaidi ya yeyote ile nyinginewe. Si moto wala chuma vilivomwendeleza binadamu.  Bali ujuzi wa matumizi yake. Vilikuwepo Kabla yake,  na wakati wake; hakuvitambua. Sasa  huo ujuzi matumizi ndio maana ya taarifa. Tunakwenda sawa? Mabibi na mabwana! Ujuzi namna, ujuzi jinsi, ujuzi vipi’ Kwa kila chenye uhai, taarifa ndio msingi wa kwanza wa kuishi;  kubakia hai hivyo kusema. Ujuzi taarifa unathibitika katika namna mbalimbali za uhai, kwenye mimea tunafahamu mmea utakuwa ukifuata upatikanaji wa mwanga, na ukiukosa utakufa, ndege na wanyama wanataratibu zao mbali mbali za kujikimu, na wanawafundisha watoto wao. Hizi zote ni namna za taarifa kwa viwango mbalimbali. Ndege ana mbawa lakini anafundishwa na zaidi yeye anajifuza kuruka, wakati unapofika Mama haleti chakula tena kiotani! Hata Paka anawafundisha watoto wake kukamata panya, kwani mtoto anaandaliwa kuendesha maisha yake mwenyewe hatimaye. Sasa kuna ghafi na ujuzi wa matumizi wa ghafi hiyo. Pia kuna ghafi binafsi mfano miili yetu, na ghafi huria, zile nyezo tuzitumiazo kwaushirikiano na viungo vyetu, kutekeleza na kufika azma mbalimbali. Ziko ghafi zionekanazo na zisizoonekana. Hivyo kusema akili kwa maana uwezo fikiri ndio ghafi kuu kuliko zote’ na kwa mujibu huo huo ubongo ndio muundo mkuu kuliko yote, kwa kutumia mawazo bongoni mwetu tunazichunguza ghafi zote na kufahamu uju-taarifa wake . Taarifa ni muundo ujuzi ndio ule ufanisi au maana, ubongo ni taarifa na mawazo ni uju-dhana kwa kadri unavyokabiliana na changamoto anuai. Inafuata kwamba binadamu ndiye kiumbe mwenye uju- taarifa wa hali ya juu kabisa, pamoja na uwezo lugha ambao ni wakipekee pia ni uju-andiko. Ni kama fani na maudhui, yini na yani, umoja na ubinafsi, mchana na usiku nk. Kitabu ni taarifa , ndani ya yale maandiko ndimo kwenye ujuzi. Mahali pa kwanza kabisa tunawajenga watu wetu kitaarifa, ndiposa Shule na maktaba  zinakuwa taasisi kubwa kabisa za ujenzi wa Taifa. Mkoa mzima wa Dar es salaam kuna maktaba moja tu, ile ya Tanganyika, tena jengo lile ni mali ya mtu,Muhindi fulani hivi. Dunia Bwana, kuna watu wao Raia wa Dunia, lakini wengine Uraia wetu ni wa zile nchi husika tuliko zaliwa tu, si penginepo. Manispaa zote za mkoa wenye orodha ya watu wasiopungua 5 millioni unamaktaba moja tu???? SASA HUO NI MJI MASHUHURI, Fikiri kuhusu mikoa  mingine, na maktaba zake moja moja kuhudumia Wilaya zote. Sio mbaya tulijaribu, lakini nchi imekuwa hii, sijaona maktaba zikiboreshwa kukidhi mahitaji ya wananchi. Nyerere alituachia urithi wa Maktaba.  Na misingi ya Elimu(Universal Primary Education) watu walifundishwa kwa muda mfupi kukidhi mahitaji ya wanafuzi, ile wanafuzi wengi walimu wachache. Alijaribu’Pongezi kwake.  Mnawaita wasomi? Mi nawaita wanataarifa visima vya uju dhana. Taarifa  inaongozwa kwa mipaka ya kufikia malengo husika, na kwa kesi yetu ni ujenzi wa Taifa. Chochote kisicho utaratibu ni wazimu na upumbavu. Swali ni : Je tunanyimwa Taarifa makusudi ilitubakie mambumbumbuu mzungu wa reliii?

nyere12Nyerere Hakuwa Daktari Kwa Andiko( Thesis) Bali Heshima’ Honorary’ zaidi ya degree 23 na tuzo nyingine za kitaaluma kutoka Vyuo na Taasisi mbali mbali kote duniani

Ametuhumiwa kukorofishana na wasomi wakati wake. Walimpa jina fulani hivi mnalikumbua? Haambiliki’ Inasemekana kwamba kila aliyejifanya anajua kuliko yeye alipata tabu katika utawala wake.  Je ndio yeye aliweka misingi ya nchi kutoongozwa na waju taarifa na dhana? Je ni wakati umefika kuvunja hii hulka? Sikubaliani na hoja hii mia kwa mia, kwani kama nilivyosema hapo awali mbona yeye mwenyewe alikuwa Mjua taarifa gwiji aliyebobea na Dunia mzima ilimtambua?? LAKINI LEO WASOMI WANAISAIDIA VIPI nchi hii? ETI KIUCHUMI ALIFELI, LAKINI KIELIMU TULIKUWA JUU, kiuadilifu, kisanaa na kimichezo,. Sasa Alifeli au alifelishwa? Elimu yake ya juu ilikwa MASTERS katika Historia na Uchumi pale Edinburgh . Alikuwa mwana taarifa gwiji huyu. Mwana Muundo jinsi asilia.

mwiny1Ali Hassan Mwinyi: Aliukata mkono wa mtoto uliochafuka kwa kulivunjilia mbali Azimio la Arusha na kutengeneza njia iliyotufikisha hapa leo’

Yaani kufa kwa Sekta ya Umma na Kuibuka kwa kizazi kipya cha vijana wa leo na Usasa, biashara ya madawa ya kulevya ikashamiri, kufa kwa Mila nyingi na Desturi za asili  kwa pamoja na ile thamani ya shilingi ya Mtanzania! Huzuni zaidi kufa kwa JKT hivyo kusababisha Taifa la vijana goigoi wasiopenda kukabiliana na majukumu na wajibu.

Nashauri basi Tuanze na maktaba, Tanzania Library Services ingewezeshwa kujenga Maktaba kila wilaya, badala ya kufanya Biashara bandia ya vyama, posho zingeelekezwa huku. Maktaba kiwe chanzo cha ajira, kwa wenye uju – taarifa mbalimbali kujitangaza. Na kuwajengea watoto ustaarabu wa kujisomea. Wajuzi wa Lugha , sanaa, na fani zingine mbalimbali, Maktaba ziwe vituo vyao vya kutoa ujuzi huu kwa wananchi kwa bei nafuu wakilipwa na Serikali na kuchangia maendeleo ya Maktaba na jamii zao kwa ujumla

maktaba1

Si tu vitabu,tujenge Maktaba Bora za kisasa zenye upatikanaji wa  huduma za kisasa za Uju undo  uwasiliani na Taarifa

Hiyo au Hizo tunazoziita dunia zilizoendelea wamefika hapo walipo kwa kujikita katika ufanisi wa ujuzi taarifa na kujenga mataifa yao katika misingi ya Adili na Kweli, hata kama kuna wakiukwaji au mapungufu lakini walishaiweka misingi! Wazungu Wazungu, ukoloni ukoloni! Mnakwenda piga shule Ulaya, mkirudi mwaja waburuza wenzenu badala ya kusaidia ujenzi wa Mataifa yenu! Watu bwana!

Mambo mazuri ya Mwalimu Nyerere yarudishwe, kwa makosa yake tujifunze, sio tena na sisi kurudia hayo hayo. Tanzania tukubali makosa yetu, kwa kuboresha miundo mbinu na miundo taarifa. Utu unajengwa kwa miundo uliomo ndani yake, kubadilisha miundo ndio kumbadilisha mtu na si vinginevyo.

Asanteni sana

* The School as The Model Of The Nation: A Contribution to the critique of Academics‘ By Gamier Mwaikoma will be released later this year.

Advertisements

4 thoughts on “MKONO UKICHAFUKA HAUKATWI

  1. kuhusu jengo la maktaba mpango ulikuwa kukodisha kwa huyo mhindi/mdosi kwa miaka kadhaa halafu lirudishwe na lote litumike kwa shughuli za maktaba lakini cha kuchekesha ni kwamba shughuli za maktaba zimebakia ground and first floor zilizobaki zote zimekodishwa kwa wachuuzi wa biashara wa kila sampuri(merchants of venice)……..

  2. ujumbe mzuri umepiga nyundo mahali pake kwenye vichwa vinavyojiita wasomi hasa hapa bongo. wamejaza phd and masters za kila sampuri lakini cha ajabu wapo bizi kugombea ubunge au kutafuta kukumbukwa kwenye post flani selekalini na darasani wapo bizi kupiga mikwara na kuvunja moyo wanafunzi inakuwa kama vile hawataki mu mwingine afike walipofika bila kuteseka
    ila

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s