Na Gamier  A. Mwaikoma

     Zitto Kabwe
Mfano wa mtu Mwadilifu Katika Wakati wetu
Sasa hivi Tanzania zile siku za uadilifu zilisha kwenda na maji! Tanzania ya sasa ni mtu pesa! Hata ukiuke taratibu gani! Kama una hela : We ndio mtu. Watu hawajali uadilifu tena kabisa! Tena waadilifu ndio wanoko wanaochukiwa na kunyanyaswa, kufanyiwa fitna na kuondoshwa. Kama huu msala wa juzi wa Zitto kabwe! Kwa utaratibu huo, CHADEMA kuna mtu pale? Au CCM NAMBA TATU? Matapiko yale yale ya mwenzio unayameza wewe? Ngoma ile ile ya Fisi, kugombania mifupa! MASLAHI YA UADILIFU KWA TAIFA NYUMA: Tumbo na kiti vimetangulia mbele. Bado ni ugomvi wa ruzuku bwana, watu hawataki kuzisamehe ili kusaidia sekta muhimu zenye bajeti finyu.
Lakini ikumbukwe kwamba uadilifu huwa unatabia moja: Au pacha au mzazi wa utu” Ndio sababu Mwalimu Nyerere alikataa habari ya watu binafsi kuwa na hela nyingiii! Wamezitoa wapi? alihoji? Kwake Baba namna pekee mtoto kuwa na hela nyingi kuliko familia ni mwizi! Aliwahi kumtia ndani kenge fulani na kumwambia wewe huwezi kuiweka serikali yangu yote mfukoni kwako” Lakini leo ni kinyume, serikali iko kwenye mifuko ya watu. Matycoon wachache tu, wanamililki vyanzo vikuu vya pato la Taifa. Sasa akisha kupa pesa zake ukapigia kampeni, tayari ameshakutia vidole” Ndio sababu Nyerere alitafuta sana kujenga ile nidhamu ya fahari ya utu. Kusisitiza nguvu ya watu/Taifa sio mtu, kwani mtu au watu fulani hata wawe nani hawawezi kuwa juu ya Taifa!
Nyerere (1)
Julius Nyerere: Pamoja na matatizo yote ya Nchi wakati wake, bado rekodi zake za taaluma , utamaduni , michezo na uadilifu ni bora na wala hazijafikiwa na wote waliomfuata
Kwani huyo Nimrodi Mkono ni nani?Si wale wale wezi ambao ndio wameushika mpini. Dr Nimrodi Mkono msomi Gwiji wa sheria lakini Mwizi. Na weza kumshabihi kwenye Fani ya utabibu na Dr wa Magonjwa ya wanawake aliyembaka mteja wake. Kuliko nidhamu, hijalishi wewe ni mtaaluma bingwa kiasi gani, utavuliwa daraja hiyo na kuswekwa ndani. Nyerere alikuwa anawapeleka kijijini waliko zaliwa kisha anaagiza wasitoke nje ya ubalozi wa nyumba kumi! Miaka ya 70 hiyo huyu mkono na Mkulo si waliiba wakakimbia nje ya nchi! Wamekuja rudi baada ya kifo cha Mzee, kusheherekea na Fisi wenzao ubakwaji wa rasilimali za hili Taifa!
Chadema wanafuata reli zile zile za CCM, NILISEMA AWALI HAKUNA JIPYA! Waadilifu hatma yao ni kama Zitto. Hakuna Haki bila mtutu wa Bunduki! Na utaratibu wa Chama ndio hiyo michezo ya Kuigiza. Kwangu mimi Zitto sasa arudi kwa watu wale aliowatumikia, kuwaelimisha na kwamba mabadiliko ni ya fikra si vinginevyo, kwa wale wanaodhani huu ndio mwisho wa kisiasa kwa Zitto hawajakosea, ni sahihi kabisa kwa maana ya wizi” Lakini Kwangu mimi ni mwanzo wa mapinduzi ya kweli. Zito awe Kamanda wa watu sasa, Na ajifunze kutoka mapinduzi ya CUBA KWAMBA ROHO YA WIZI( KWA MAANA YA UBEPARI: HAIFI KWA URAHISI) Ambapo VIONGOZI NA SERIKALI ZA NCHI zikihongwa na mashinikizo ya nchi zilizoendelea kufanya kazi kwa maslahi ya wao.

Guevara na Castro
Walithibitisha kusimama kwa ajili ya haki ni vita 

 Zitto na kuomba umrejee Che Guevara, safari ya mapinduzi ya kweli ni Ngumu, ni baina ya haki UZIMA na kifo! Akiwa na umri karibu sawa na wako: miaka 39″ mwezio alikuwa vitani na kufa akipigana kuiondoa serikali ya wezi ya Bolivia katika kampeni yake ya kuikomboa Amerika ya kusini dhidi ya unyonyaji wa Kaskazini. Tupo tunakuangalia Zitto, tunakusubiri uanzishe mtando usio na chama wa kumkomboa mtanzania kifikra na wanamtandao huu ni wote watakao jitolea kuikomboa Tanzania.
Uwike Usiwike: Kutakucha! Msichoke watoto mapambazuko karibu”
Images copyright
1. Zitto Kabwe:
Che and Fidel
Photo from The New York Times Photo Archives:
Advertisements

2 thoughts on “Fahari ya Uadilifu

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s